Akiwa amevua shati huku akiwa anaombewa akiwa eneo la kanisa.  Jamaa  alikuwa akijihusisha na vitendo vya kishirikina, akiwa chini ya wanamaombi wa kanisa la Ufufuo na Uzima Arusha mara baada ya mtu huyo kukamatwa usiku wa kuamkia leo wakati wa maombi kanisani hapo ambapo ametoa maelezo mbalimbali namna alivyokuwa akishiriki katika vitendo hivyo vya kishirikina.


Vitenda kazi vyake vikiwa vimemwagwa chini. 




Vitendea kazi vya jamaa

Katika hali isiyo ya kawaida mtu huyu ajulikanaye kwa jina la Shabani Hamis amenaswa akiwa anafanya uchawi katika kanisa la Ufufuo na Uzima Arusha.


Matukio ya kunaswa wachawi yamekuwa mengi kanisani hapo kutokana na uweza wa Mungu unaojidhihirisha kupitia Mchungaji Kiongozi wa kanisa hilo, Frank Andrew.


Pamoja, na kukutwa bila nguo mtu huyo aliyekuwa amebeba vifaa ambavyo kwa mujibu wa maelezo yake, huvitumia kuwanga na kupaa ni pamoja na tunguli na kikapo cha mkoba wa uchawi. Tukio hilo la aina yake limetokea Usiku wa saa sita, wakati mkesha wa maombi ukiendelea kanisani hapo.


Baada ya maombi makali ya kuharibu uchawi katika anga la Arusha, ikafuatiwa na tukio hilo. Mungu ni mkuuu maana hapana uchawi wala Uganga juu ya watu wa Mungu.

0 comments:

Post a Comment

 
Top
Blogger Template