BUKOBA HAPAKUWA NA NDEGE WA AJABU YASEMA SERIKALI!
SERIKALI ya Wilaya ya Bukoba Mkoani Kagera imetoa ufafanuzi wa Ngege waliokuwa wanadaiwa kutoa Kinyesi cha ajabu katika Kisiwa cha Msira, na kusababisha Vifo vya Kuku 516 na Mbuzi 12 wanaodaiwa kugusa au kula kinyesi chao kuwa ndege hao hawakuwa na madhara ya aina yeyote.
Afisa Tarafa wa Kata ya Rwamishenye katika Manispaa ya Bukoba, Abdon Kahwa, akizungumza na FIKRAPEVU kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya hiyo, Ziporah Pangani, alisema kuwa Serikali kupitia Wizara ya Mifugo Kanda ya Ziwa, imefanya uchunguzi wa kina na kubaini kuwa Ndege waliokuwa wanahisiwa kuwa ni wa ajabu sio kweli kwani ndege hao walikuwepo katika kipindi cha muda mrefu kisiwani hapo.
Hata hivyo alisema ndege hao aina ya ‘Nyange nyange’ ambao wana rangi nyeusi na nyeupe, hawakuwa na madhara kama ilivyokuwa imeripotiwa hapo awali katika Vyombo vya Habari ikiwemo mitandao ya Kijamii Machi 12, mwaka huu, ambapo madhara yaliyojitokeza 'magonjwa ya mifugo' yalisabababishwa na uchafu wa ukosefu wa Vyoo na maji pamoja na ugonjwa wa kawaida unaopata mifugo.
Aidha, amesema Wataalamu kutoka Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii na Wizara nyingine zinazohusika, katika utafiti wake chanzo cha ndege hao kunya kinyesi kilichoitwa kuwa kina sumu, hakikuwa na madhara, wataalamu hao walipima mifupa ya kuku waliodaiwa kufa kwa ajili ya kinyesi hicho bila kuona ugonjwa wowote uliokuwa umetajwa kuwa ni wa ajabu.
“Timu iliyotoka Wizara ya Mifugo kanda ya Ziwa, ilifuatilia na kufanya upasuaji kwenye mifupa ya Kuku na kubaini kuwa, Kuku waliokufa inatokana na magonjwa ya kawaida kwa Kuku yanayosababishwa na Vairasi protozoa, na bacteria, ambao ndio walisababisha kuku kufa” alisema Kahwa
Amesema Wataalamu hao walitibu Mifugo hiyo na Kuku waliobainika kuathiriwa na Ugonjwa huo 'magonjwa ya mifugo', kwa kutumia dawa za kawaida, na kukanusha kuwa hakuna vifo vya Kuku 516 vilivyotokana na ugonjwa ndege aina ya ‘Nyange nyange’.
“Hii ni kuwa jamii nyingine ya Mabata Kanga haijadhurika, Mizoga ya Kuku na Mbuzi ilifanyiwa utafiti hivyo ilivyosemekana kuuwa kuku 516, mbuzi wawili kufa ni tofauti na tulivyoona hivyo hatukubaini kuwa kuna ugonjwa mwingine tusioujua, bali ni ugonjwa wa kawaida” alisema Kahwa
Awali iliripotiwa kuwa wapo ndege wa ajabu waliosababisha hofu kwa wakazi wa Kisiwa hicho, ambao wanaokunya kinyesi cha ajabu kinachosababisha kutu kwenye Mabati na kusababisha yatoboke kwa muda mfupi na kusababisha Kuku na Mbuzi kufa katika Kisiwa hicho.
0 comments:
Post a Comment