Ilikuwa Mida ya Saa tatu za asubuhi ambapo Magari zaidi ya 10 ya Jiji yalikuwa yamejipanga eneo la mwenge Huku kukiwa na Ma Askari wa FFU wa kutosha pamoja na Migambo wa Jiji huku wakiongozwa na watu wa Jiji kwa ajili ya Kukamilisha swala zima la bomoa bomoa vibanda vyote ambavyo havina mpangilio. 
 Mgambo wakiondoa mikokoteni na kuipakia kwenye gari bada ya kufanya zoezi zima la bomoabomoa eneo la Mwenge jijini Dar es Salaam. Zoezi hilo lilianza kwa utulivu na kuendelea kwa utulivu kutokana na ulinzi mkubwa uliokuwepo huku wananchi wakiendelea na kazi zao kama kawaida na kukatazwa kukatiza katika eneo la tukio kwa usalama wao


Hata hivyo Baada ya vibanda hivyo kutolewa kumegundulika kuwa kulikuwa ni kuchafu kupindukia kutokana na uchafu uliokuwa umezagaa kila kona.
 Kulia ni Magari mbalimbali ya Serikali yakiwa yamepaki eneo la Mwenge huklu zoezi likiendelea
Hili ni eneo la ndani ya Mwenge ambapo wamebomoa  vibanda vyote
 Akina Mama eneo la Mwenge wakihangaika kutoa vitu vyao baada ya Bomoa Bomoa kupita..Hawa ni wale wauza Chai na Supu asubuhi na hata chakula cha mchana
 Huwezi amini lakini ndio hali halisi sasa eneo jirani na Kituo cha Mabasi Mwenge hakuna tena Adha ya vibanda , lakini umebaki uchafu uliopitiliza na kugundulika kuwa hawa watu walikuwa wakifanya Biashara katika maeneo ambayo si salama
 Hili ni eneo ambalo lilikuwa ni maarufu kwa ajili ya kuuza vitu mbalimbali kama nguo na viatu vya mitumba lakini kwa sasa hakuna kitu ni peupe
 wakiendelea kukusanya mabaki ya Mabanzi katika eneo hilo la mwenge

 
 Kwa wale akina dada hili lilikuwa eneo maarufu sana kwa ajili ya Kutengenezea nywele na saloon bubu ambazo zote zimevunjwa vunjwa kwa sasa
 Hapa juu mwanzo kulikuwa na mabanzi ya kutosha na wakina dada wengi walikuwa wanapenda kuwa hapa wakitengenezwa nywele zao wasijue kuwa walikuwa wakikaa katika eneo chafu kama hili.
 Gari hili likijiandaa kuondoka baada ya somba somba
 Kwa kuliangalia Eneo hili utasema ni chafu sana lakini ndio ambalo lilikuwa maarufu hasa kwa akina mama na akina dada kutengenezea kucha zao na kusuguliwa miguu, Je kama wangejua ni pachafu hivi wangeweza kugusa hata kuja kutengeneza kucha?
 Bomoa bomoa ikiendelea
 Baada ya kufanya manunuzi watu hutupa takataka tuu, zilikuwa zikijificha kulingana na mkusanyiko wa watu lakini hii ndio hali halisi sasa

 Hakuna Vibanda lakini adha imebakia sasa ni ya uchafu
 Je hapa tutapona magonjwa ya mlipuko?
Sehemu hii ya stendi ya Mwenge ni peupe kuna nafasi ya watembea kwa miguu

 Huu ni upande wa pili wa kuelekea Mikochemi ambapo bajaji Hupaki napo wamesafisha kwa kubomoa vibanda vyote hapa ni Shwari peupe
 Picha hizi mbili ni eneo maarufu sana ambapo watu walikuwa wanauza Vifaa vya umeme na DVD, Sub Woofer pamoja na Radio bila kusahau TV sasa pamebaki kama hivi, Je walikuwa hawajui kama ni pachafu kiasi hiki?

Picha na Pamoja Blog/ Dar es salaam yetu Blog

0 comments:

Post a Comment

 
Top
Blogger Template