Kutokana na mvua zinazonyesha hivi sasa kwenye jiji la Dar es salaam zimesababisha mambo mengi kusimama pamoja na miundombinu kuharibika hasa madaraja yanayounganisha njia kuu.

Nyumba nyingi zimeingia maji hasa maeneo ya mabondeni na kulazimisha familia kuhama kutoka kwenye makazi yao. Kamanda Kova amethibitisha kutokea kwa vifo vya watu kumi watoto watano na watu wazima watano kutokana na mafuriko haya.
Kamanda Kova amesisitiza kwamba hali sio nzuri wananchi wanatakiwa wachuke tahadhari kwenye makazi yao na hata wanaotembea na vyombo vya moto barabarani kwasababu njia nyingi zina mashimo.
Kamanda Kova anasema pia watu wapunguze mizunguko isiyo lazima na kutulia kwenye makazi yao ili kuepusha madhara mengine kutokea.
Hizi ni baadhi ya picha kati ya nyingi zinazosambaa kwenye mtandao.


0 comments:

Post a Comment

 
Top
Blogger Template