Naomba niombe msaada kwenu wadau,nina matatizo sijui niseme shida  ambazo kiukweli zinanikosesha raha,nimekua nikihangaika sana kutafuta dawa ya kumaliza harufu ya kikwapa,yaani ni kwamba nimejaribu kila aina ya deodorant,na perfumes za kila aina lakini harufu haiishi,itokee bahati mbaya nisahau kupata Deodorant jamani sio siri najisikia hata mimi mwenyewe jinsi ninavyotoa harufu kali,zaidi ya harufu makwapa yangu ni meusi,ajabu,niliambiwa deodorant za Forever Living zinasaidia kumaliza weusi makwapani lakini wapi sioni tofauti,nawaombeni mnisaidie jamani nakosa raha,kifupi harufu utadhani lile jasho wanalonuka wanaume,wakati mwingine nafikia hata kujinyanyapaa mwenyewe,kwa kutokwenda kwenye shuhuli,nahisi wenzangu wananisema,shida inakuja muda wa kazi,kwani siwezi kukwepa kwenda ofisini,kiukweli it is so embarrassing.

La pili,huohuo weusi,katikati ya mapaja nako hakufai,yaani nikipanua miguu utadhani nimesilibwa lami hapo kati,nimejaribu kutumia mikorogo,haikusaidia,cream zile za hospitali za ngozi,pia nimejaribu,angalau kidogo utaona natakata,tatizo lake baada ya muda yanatoka mapele kama vijipu nashindwa hata kutembea shauri ya friction,nilipata ushauri wa kuvaa skin tight ili kuepusha friction,lakini lile la weusi lipo palepale,wenzangu nawaomba,kama kuna mtu alishawahi pata  matatizo kama yangu,naomba msaada tutani,jamani siyo siri,pamoja na kutaka nionekane maridadi,lakini pia wakati wa majambos si mwajua kuna muda wa mahabuba kwenda down,sasa inapofikia hapo,dah,najisikia aibu kwa maana naona kama vile najichoresha,na jamaa yangu huwa hakubali bila kunipagawisha kwa njia hiyo,sasa nipo na wakati mgumu
.
Huwa napendelea sana kusoma story kila wikiendi ila wamama/wadada saa nyingine mna maneno makali ambayo yanatukatisha tamaa kuomba ushauri humu,nawaombeni jamani,wengine hatuna pa kusemea wala wa kutupa ushauri wa kweli,tusaidiane jamani,Samahani kama nimewakwaza

0 comments:

Post a Comment

 
Top
Blogger Template