PICHA NA TAARIFA:LORI LA MAFUTA LALIPUKA DAR, WAWILI WAJERUHIWA
Mafundi wa Kampuni ya Oilcom wakiangalia mabaki ya lori la kampuni hiyo lililochanika baada ya kulipuka kwa tanki lake wakati likichomewa katika eneo la Tabata Relini, jijini Dar es Salaam jana. PIcha na Emmanuel Herman
Taharuki ya aina yake ilitokea jana eneo la Tabata Relini kwenye yadi ya malori ya Kampuni ya Oilcom baada ya kutokea kishindo kikubwa kilichotokana na kupasuka kwa tanki la mafuta
Tukio hilo lililotokea saa 11 jioni, lilizua hofu miongoni mwa wakazi na wafanyakazi wa eneo hilo, na lilitokana na hitilafu ya kiufundi wakati wa kulitengeneza tanki hilo.
Mashuhuda wa tukio hilo lililojeruhi watu watatu waliliambia Mwananchi kuwa mlipuko huo ulitokea wakati fundi akichomea sehemu ya tanki katika karakana ya magari ya kampuni hiyo.Kwa habari zaidi
0 comments:
Post a Comment