Rob Kardashian ambaye ni mdogo wa kiume wa mwanamitindo Kim Kardashian amedaiwa kuitosa sherehe ya kufunga ndoa kati ya dada yake na Kanye West itakayofanyika May mwaka huu jijini Paris, Ufaransa kwa kuwa haufurahii muonekano wake.
“Rob amekasirika na hayafurahii mabadiliko ya muonekano wake na kwa kweli anajisikia kama yeye ni kondoo wa familia yao.” Chanzo kimoja kiliiambia RadarOnline.
Chanzo hicho kilieleza kuwa Rob na Kim wanapendana sana, lakini Rob anajisikia kama akiwa kwenye tukio hilo ambalo litawajumuisha watu mbalimbali maarufu, atakuwa kama amewekwa kando na kuchukuliwa kama hahusiki moja kwa moja.
Hivi karibuni Rob aliripotiwa kutafuta msaada wa matibabu kwa ajili ya uzito wake ulioongezeka baada ya kugundua kuwa akiendelea kuongezeka atakuwa katika hatari ya kupata magonjwa.

0 comments:

Post a Comment

 
Top
Blogger Template