KUJENGEA MAKABURI YA WALIOTUTANGULIA - KUNA UMUHIMU WOWOTE?
Habari za asubuhi ya leo wapendwa wana Jamvi....
Kwanza niombe radhi kwa nitakaowakwaza kwa namna moja ama nyingine.
Kuna suala hili huwa linanitatiza naomba kuelewesha.
Kumezuka tabia ya kujengea makaburi kwa marumaru ya samani za aina tofauti tofauti tena zenye gharama kubwa, Utakuta mtu alikuwa anaumwa kwa muda mrefu lakini watu hawakujitokeza kumhudumia lakini baada ya mtu huyo kufariki dunia wanajitokeza ndugu, jamaa na marafiki wanapanga mipango ya kujengea kaburi lake na kuweka nakshi ya kila aina.
Je watu hawa walikuwa wapi wakati wa ugonjwa??
Je kujengea kaburi hilo kutamsaidia nini yule marehemu??
Kuna watu wanafariki ghafla aidha kwa ajali ama kifo cha aina yoyote ila kwa ghafla... Kuna ulazima gani wa kulinakshi kaburi???
Tena kuna wengine wamekwenda mbali wakaanza kutafuta makaburi haya ya mababu zao na kuanza kuyajengea na kuyaweka katika hali ya unadhifu kana kwamba kilichomo ndani yake kina thamani... Tena na kufanya sherehe sijui ya kujengea makaburi... Ni nini maana yake???
Kwa mtazamo wangu ujenzi huu wa kuweka nakshi ni kugharamika kusiko na faida...
N.B. Ni mtazamo tu naomba nisipondwe mawe....
0 comments:
Post a Comment