KITU GANI KINAMFIKISHA MTU KWENYE UFANISI KATIKA MAISHA
Nimeshakutana na wasomi kila aina,lakini majority yao ni watu wasiokuwa na uwezo hata wa kuendesha maisha yao.Na nimeshakutana na watu wasiokuwa na elimu ya maana...lakini ni watu makini,wana uwezo wa kifedha,wanajiamini na wanaendesha shughuli zao vizuri.
Sasa labda hapa ni kutafuta sababu za hawa wasomi kuwa watu wa vitabu,data,laptop,kuendesha semina n.k lakini wakawa dhaifu inapofika suala la kutajirika,kuwa na mamlaka na kujiamini.
Mfano ni fundi viatu wa miaka ya sitini Said Salim Bakhressa maarufu kwa ice cream na bidhaa tofauti hapa nchini.AU hata Billy Gates..aliyekimbia shule akiwa grade 10...na sasa ni mmoja ya matajiri wakubwa duniani.List yao ni ndefu...kina Ford..n.k.
Je ni kitu gani cha ziada ambacho wasiokuwa na elimu ya juu...walichonacho hadi wakafanikiwa katika malengo yao,ambacho hakipatikani kwa wenye Phd..n.k?
0 comments:
Post a Comment