MSANII wa filamu za Kibongo, Kajala Masanja hivi karibuni alionesha jeuri ya magari baada ya kutinga nayo mawili kwa nyakati tofauti kwenye kumbukumbu ya miaka miwili ya marehemu Steven Kanumba.
Awali kwenye ibada ya kumuombea marehemu, Kajala alifika kwenye kanisa moja lililopo
Kimara Temboni akiwa ‘anadraivu’ gari aina ya Toyota Harrier nyeusi na kuzua gumzo eneo hilo
Baadaye msafara ulipohamia Makaburi ya Kinondoni alipozikwa Kanumba, alitinga na gari lingine aina ya Toyota Brevis lile ambalo ilidaiwa kuwa alinunuliwa na yule kigogo wa shosti wake, Wema Sepetu anayejulikana kwa jina la CK. Jeuri hiyo iliwafanya wengi kubaki na vingi viulizo na Ijumaa lilipojaribu kumdadisi hakutoa ushirikiano na hata alipopigiwa simu baadaye hakupatikana hewani
0 comments:
Post a Comment