Mbwa  anayenyonyesha  watoto  wa Nguruwe Iringa anaitwa Asha 


Mchungaji    Daniel  Kisonga akimwonyesha  mbwa anayeitwa Asha ambae  ananyonyesha  watoto wa Nguruwe  
 Mbwa  huyo akinyonyesha  watoto wa Nguruwe  huku mtoto  wake (kulia) akishindwa  kunyonya
 Huyu  ndie Mbwa anayenyonyesha  watoto  wa Nguruwe  Iringa

Katika  hali  isiyo  ya  kawaida kuzoeleka  ni baada ya  wakazi  wa Ilala katika Manispaa  ya Iringa  leo kushuhudia maajabu ya  dunia baada ya  kushuhudia tukio la aina yake kwa mbwa  kuwachukua  watoto  wa nguruwe  na  kuwalea  kwa  kuwanyonyesha maziwa  yake.
Tukio  hilo  limetrokea  jana asubuhi  baada ya  nguruwe  wa mmoja kati ya  watumishi  wa mungu (mchungaji ) Daniel  Kisonga  kushuhudia mbwa  huyo ambae  alikuwa amezaa  watoto  watatu  na kufariki  wawili na kubakia na mtoto mmoja na hivyo  kulazimika  kuingia katika banda la nguruwe na kubeba  watoto  wanne wa nguruwe na kuamua kuwalea na kuwapa  huduma  zote  ikiwemo ya  kuwanyonyesha kwa upendo  watoto hao  wa Nguruwe  bila  kuwadhuru.
Akizunguza  na  mwandishi  wa habari  hizi  leo mchangaji Kisonga amesema  kuwa ni vigumu kuamini kuna  mbwa  akinyonyesha  watoto  wa nguruwe wakati kwa kawaida  mbwa amekuwa ni mnyama hatari  kwa  nguruwe hao hasa  pale  wanapozaliwa  .
Amesema  kuwa  mbwawa wamekuwa wakiingia katika mazizi ya nguruwe na kuwala nguruwe hao baada ya kuzaliwa ili imekuwa tofauti kwa mbwa   huyo anayeitwa Asha baada ya  kuamua  kulea  watoto  wa nguruwe .
Hata  hivyo amesema yawezekana ni maajabu ya dunia ila pia yawezekana ni  dalili za  siku ya mwisho kama ambavyo zimepatwa  kutabiliwa katika maandiko matakatifu kuwa  siku za mwisho yatajitokeza mambo mengi ya ajabu ambayo  binadamu ni vigumu kuamini mambo hayo.
Japo  upande wa  wadau mbali mbali wamehoji  nguruwe hao iwapo wataendelea  kunyonya maziwa na mbwa  wataliwa na binadamu ama lah !  kutokana na nyama ya mbwa kwa kawaida  kutoliwa na binadamu  sasa  iweje kwa  nguruwe hao  kunyonya maziwa ya mbwa.

0 comments:

Post a Comment

 
Top
Blogger Template