Tuache tunasoma bwana wewe!: Wananchi wakimuangalia mgambo wa Manispaa ya Ilala wakati akichukua magazeti katika moja ya meza maeneo ya Posta mpya jijini Dar es Salaam leo.Mkoa wa Dar es Salaam upo katika operesheni kabambe ya kusafisha jiji kwa kuwaondoa wafanyabiashara wanaofanya biashara ndogo ndogo maeneo yasioruhusiwa wilaya zake zote za Ilala, Temeke na Kinondoni.
Mgambo wa Manispaa ya Ilala akiwa amebeba magazeti.Mgambo wakiondoa kibanda cha Kampuni ya Simu ya Tigo.
Ooh! Hamtaki kuondoka?: Askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU), wakiimarisha ulinzi wakati wa oparesheni hiyo.
Ooh! Hamtaki kuondoka?: Askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU), wakiimarisha ulinzi wakati wa oparesheni hiyo.
Katika hatua nyingine, nao wafanyabiashara wadogo wadogo stendi ya mabasi ya abiria ya Mwenge wamekumbwa na kadhia hiyo kama inavyoonekana katika picha za chini
Kweli jamani?: Wafanya biashara wa Stendi ya Daladala Mwenge jijini Dar es Salaam wakiwa hawana lakufanya wakati zoezi la bomoa bomoa likiendelea
Thubutu kuleta fujo: Askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU), wakiimarisha ulinzi wakati wa oparesheni hiyo.Hili nalo si mahala pake: Mgambo akiondoa moja ya toroli eneo la Mwenge.Usilete mchezo: Askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU), wakiwa kwenye doria.Lazima utulie: Askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU), wakiwadhibiti wafanya biashara eneo la Mwenge jijini Dar es Salaam.
PICHA ZOTE NA PHILEMON SOLOMON WA FULLSHANGWE DAR ES SALAAM
0 comments:
Post a Comment